Monthly Archives: February 2015
Klabu ya ES Setif yabeba Makombe yote ya Afrika mwaka 2014/2015….yachukua pia CAF SUPER CUP
Klabu ya Algeria ES SETIF ndo BINGWA wa CAF Super Cup. CAF Super Cup ni mchuano unaowakutanisha mshindi wa Bingwa Klabu Bingwa Afrika na Bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika. ES Setif ilikuwa ikicheza na Al Ahaly ya Misri katika uwanja wa Mustapha Tchaker. Kwa mwaka 2014/2015 ES Setif imeweza kuchukua Ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika na hili CAF Super Cup. ES Setif iliishinda klabu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kongo kwa goli la ugenini katika Fainali za Klabu Bingwa Afrika mwishoni mwa mwaka 2014.

Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi daraja la kwanza kupigwa kesho Chamazi, Mwadui na African Sports kuumiza nyasi
Dar es Salaam:
Fainai za Kumsaka bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kupigwa kesho jumapili saa 10 Jioni kwa saa za hapa Tanzania. Mchezo huo ulitakiwa ufanyike uwanja wa Taifa, lakini Shirikisho la Soka Tanzania TFF limesema kuwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake mchezo utapigwa uwanja wa Chamazi.
Mchezo huo unatarajia kurushwa LIVE na kituo cha AZAM TV ili kuwafikia watu wengi mikoa mpambano huu mkali. Kinara ama Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza atajinyakulia kombe pamoja na medali, huku mshindi wa 2 atajipatia kikombe na medali pia.
Viingilio vya mchezo huo ni Tsh. 5,000 kwa jukwaa kuu na Tsh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.
Mwadui FC inashikilia msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza kundi la B ikiwa na pointi 46 katika michezo 22, huku African Sports inapointi 48 katika michezo 22 na yenyewe ikiwa ni kinara wa Ligi Daraja la Kwanza kundi A.
Aston Villa yamtaja Tim Sherwood kuwa kocha wao mpya

Bwana Tim Sherwood atajwa na Klabu ya Aston Villa kuwa kocha wao hii leo mapema. Klabu hiyo ya Uingereza imeingia mkataba na bwana Tim mpaka 2018.
Bwana Tim Sherwood miaka 46 alikuwa kocha wa Tottenham mwaka 1999–2003. Bwana Tim amemrithi aliyekuwa kocha wa Aston Villa bwana Paul Lambert. Paul Lambert alifukuzwa na klabu hiyo kwasababu ya matokeo mabovu Ligi Kuu Uingereza. Aston Villa siku ya Jumanne mwezi huu wa February walipigwa na Hull City 2-0 ambapo illikuwa ni mechi ya 10 mfululizo katika ligi bila kushinda chini ya Paul Lambert. Bwana Tim Sherwood anaichukua Aston Villa ikiwa ipo nafasi ya 18 katika mstari wa kushuka daraja Ligi Kuu Uingereza na Pointi 22 katika michezo 25.
Kigogo mwingine Azam FC amfunza adabu Mtibwa Sugar
Dar es Salaam:
Azam FC ama wanaramba ramba wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa kishindo cha kuibamiza Mtibwa Sugar goli 5-2 katika kuwanja wa Chamazi Complex Jijini Dar es Salaam. Kwasasa Azam FC inashikilia Ligi kwa pointi 25 katika michezo 13 sawa na Yanga. Azam inamzidi Yanga idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga.
Hadi Mapumziko Azam FC walikuwa mbele kwa Bao 3-1 kwa Bao za Kipre Tchetche, Frank Domayo na Didier Kavumbagu huku Bao la Mtibwa Sugar likipachikwa na Musa Nampaka. Kipindi cha Pili, Domayo akaipa Azam Fc bao la 4 na Amer Ali kuipa Mtibwa Bao lao la Pili lakini Kipre Tchetche akawakata maini na kupiga Bao la 5 na kuifanya Gemu imalizike 5-2.
Ligi Kuu Vodacom itaendelea Wikiendi kwa Mechi kadhaa bila ya Azam FC na Yanga kushiriki kwa vile wana Mechi za Klabu Barani Afrika za Mashindano ya CAF. Ligi kuu itaendelea wiki hii siku ya jumamosi ( Ndanda FC V Mtibwa Sugar, Coastal Union V Mbeya City na Stand United V Mgambo JKT) Yanga wao siku ya Jumamosi hii tarehe 14/2/2015 itawakaribisha nyumbani Tanzania Uwanja wa TAIFA klabu ya BDF IX ya Botswana katika Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho Afrika ama Confederation Cup. Wakati Azam wao watawakaribisha Mabingwa wa CECAFA El Merreikh ya Sudan hapa Tanzania Uwanja wa Chamazi Complex siku ya Jumapili tarehe 15/2/2015.
Kocha wa Aston villa Paul Lambert apigwa CHINI
Klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza Aston Villa imempiga chini kocha wake bwana Paul Lambert. Klabu ya Aston Villa imetangaza kwenye ukurasa wake wa mtandao kuwa imeamua kuachana na kocha huyo na kwamba bwana Scott Marshall na kocha wa ,magolikipa Andy Marshall watachukua mikoba kwa mda huu ambao klabu itakua ikitafuta kocha mwingine. Klabu hii inaenda kucheza mchezo wa kombe la FA na Leicester City jumapili hii katika uwanja wa Villa Park.
Aston Villa siku ya Jumanne alipigwa na Hull City 2-0 ambapo ni mechi ya 10 mfululizo katika ligi bila kushinda. Aston Villa kwasasa ipo nafasi ya 18 na ina pointi 22 tu katika Ligi Kuu Uingereza.




