Daily Archives: February 4, 2015
Kocha Hervé Renard Aipeleka Ivory Coast FAINALI za Kombe la Matiafa Afrika 2015 tena
Ivory Coast imetinga katika Fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2015 kwa kuitwanga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo goli 3 – 1 katika uwanja wa Bata. Ivory Coast sasa itakutana na Mshindi wa kati ya Equatorial Guinea na Ghana ambao watacheza tarehe 5/2/2015. Fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2015 zitapigwa siku ya Jumapili ya tarehe 8 mwezi huu
Ilikuwa ni vita ya Wafaransa wawili kocha J. Ikwanga-Ibenge na Herve Renard. Mechi ilikuwa ikitazamiwa kuwa ya ushindani mkubwa sana ukilinganisha uwezo wa wachezaji Bolasie, Mbokani, Makiadi na Bokila wote wa Kongo pamoja na mastaa wa Ivory Coast kama Gervihno, Bony, Yaya Toure na Kanon.
Mpira ulianza kwa lango la Kongo kushambuliwa kutoka kwa winga Gevihno na upenyo wa Yaya Toure. Akipokea pasi kutoka kwa Bony, Yaya Toure akafungua kalamu ya magoli dakika ya 20 kwa kukunjuka shuti lililokuwa linakadiliwa kuwa na spidi ya kilomita 125 kwa saa lililomshinda mlinda mlango wa Kongo Kidiaba, na mda mfupi dakika ya 22 Kongo wakapata penati iliyowekwa wavuni na Dieumerci Mbokani. Nae mchezaji wa zamani wa Arsenal Gervihno akapokea pasi kutoka kwa Wilfred Bony na akatupia la pili (2) dakika ya 40 likiwa pia ndo goli lake la 20 kwa Ivory Coast. Na kama haitoshi beki Serge Wilfried Kanon akashindilia msumari wa 3 ulioongezea kuwapeleka Ivory Coast kama Taifa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2015 huko Bata.
YANGA YAPANDA KILELENI MWA LIGI!
Yanga ama vijana wa Jangwani leo hii wamecheza mchezo wao wa 12 wa Ligi kuu Tanzania Bara. Yanga wamewafuata Tanga, Coastal Union leo hii na kuibuka na ushindi finyu wa goli moja kwa nunge katika uwanja wa Mkwakwani. Goli la Yanga limewekwa wavuni na Nahodha wao Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika dakika ya 12 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo. Ushindi huu umeifanya Yanga ikae kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 22 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 21 na inayaoshikilia nafasi ya tatu ni Mtibwa Sugar yenye pointi 18. Azam FC na Mtibwa Sugar wao washacheza michezo 11 kila moja.


