Daily Archives: February 5, 2015
Bingwa mara 4 wa Kombe la Mataifa Afrika atinga Fainali kwa kumpa kipigo kwake Equatorial Guinea kwa Vujo!
Kutoka Uwanja wa Malabo nchini Equatorial Guinea, mechi iliyokuwa inachezwa ni ya nusu fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2015. Mechi kati ya wenyeji Equatorial Guinea dhidi ya Ghana imemalizika kwa ushindi wa mgeni Ghana wa 3 kwa nunge. Ushindi uliosababisha Ghana kutinga fainali za Mataifa Afrika 2015 na atakutana na Ivory Coast hiyo Jumapili.
Ghana ni mabingwa wa Kombe hili mara nne kwa miaka ya 1963, 1965, 1978 na 1982, pia hii ni mara yao ya tano wanatinga Fainali hizi kwa miaka ya 1968, 1970, 1992, 2010 na sasa 2015. Ghana sasa kukipiga FAINALI na Ivory Coast siku ya Jumapili tarehe 8/2/2015 saa 4:00 usiku. Ivory Coast wao ni washindi wa kombe hili la Mataifa Afrika mara moja mwaka 1992 na wameshatinga fainali mara 3 mwaka wa 2006, 2012 na sasa 2015.
Dume lingine ya Uhispania, Barcelona kubadilisha jina la Uwanja wake Nou Camp
Uwanja wa klabu ya Barcelona unaweza kuja kubadilishwa jina lake la sasa Nou Camp hapo baadae. Mkataba na mdhamini wa Barcelona Qatar Airways unaenda kuisha mda wake mwaka 2016 ambao unathamani ya paundi milioni 25 kwa mwaka . Klabu ya Barcelona inayopatikana katika jimbo kubwa Catalunya nchini Uhispania hivi karibuni itafanya makubaliano na Qatar Airways ili kuongeza mkataba.
Mkurugenzi Mtendaji ama kwa kingereza CEO wa shirika la ndege la Qatar Airways amesema kuwa katika mkataba huo mpya jina la uwanja linaweza kubadilika kidogo kwa kuongezea maneno. Mkurugenzi wa shirika la ndege la Qatar, Bwana Akbar Al Baker ameendelea kusema kuwa katika mkataba huo jina la kampuni yaani QATAR linaweza kuongezwa kwenye jina la Uwanja Halisi NOU CAMP.


