Daily Archives: February 9, 2015
Ivory Coast Bingwa Kombe la Mataifa Afrika 2015
Bata:
Ivory Coast ndo MABINGWA wapya wa Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2015. Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika 2015 yalifikia tamati katika uwanja wa Bata, Equatorial Guinea. Fainali hizi za tarehe 8/2/2015 zikiwakutanisha miamba wa Afrika Ghana na Ivory Coast wakimaliza dakika 120 za mchezo na kuingia katika mikwaju ya penati. Golikipa wa Ivory Coast Boubacar Barry ndo alionekana kama Mfalme wao baada ya kudaka penati ya kipa wa Ghana Brimah Razak kupiga penati ya mwisho iliyomshinda kipa wa Ivory Coast.
Ivory Coast ilishinda kwa penati 9 kwa 8 dhidi ya Ghana baada ya kumaliza dakika 120 za mchezo. Historia imejirudia ambapo Ivory Coast walishinda kwa penati 11-10 dhidi ya hawa Ghana. Hili ni kombe la pili la Ivory Coast kushinda.


