Daily Archives: February 11, 2015
Kigogo mwingine Azam FC amfunza adabu Mtibwa Sugar
Dar es Salaam:
Azam FC ama wanaramba ramba wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa kishindo cha kuibamiza Mtibwa Sugar goli 5-2 katika kuwanja wa Chamazi Complex Jijini Dar es Salaam. Kwasasa Azam FC inashikilia Ligi kwa pointi 25 katika michezo 13 sawa na Yanga. Azam inamzidi Yanga idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga.
Hadi Mapumziko Azam FC walikuwa mbele kwa Bao 3-1 kwa Bao za Kipre Tchetche, Frank Domayo na Didier Kavumbagu huku Bao la Mtibwa Sugar likipachikwa na Musa Nampaka. Kipindi cha Pili, Domayo akaipa Azam Fc bao la 4 na Amer Ali kuipa Mtibwa Bao lao la Pili lakini Kipre Tchetche akawakata maini na kupiga Bao la 5 na kuifanya Gemu imalizike 5-2.
Ligi Kuu Vodacom itaendelea Wikiendi kwa Mechi kadhaa bila ya Azam FC na Yanga kushiriki kwa vile wana Mechi za Klabu Barani Afrika za Mashindano ya CAF. Ligi kuu itaendelea wiki hii siku ya jumamosi ( Ndanda FC V Mtibwa Sugar, Coastal Union V Mbeya City na Stand United V Mgambo JKT) Yanga wao siku ya Jumamosi hii tarehe 14/2/2015 itawakaribisha nyumbani Tanzania Uwanja wa TAIFA klabu ya BDF IX ya Botswana katika Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho Afrika ama Confederation Cup. Wakati Azam wao watawakaribisha Mabingwa wa CECAFA El Merreikh ya Sudan hapa Tanzania Uwanja wa Chamazi Complex siku ya Jumapili tarehe 15/2/2015.
Kocha wa Aston villa Paul Lambert apigwa CHINI
Klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza Aston Villa imempiga chini kocha wake bwana Paul Lambert. Klabu ya Aston Villa imetangaza kwenye ukurasa wake wa mtandao kuwa imeamua kuachana na kocha huyo na kwamba bwana Scott Marshall na kocha wa ,magolikipa Andy Marshall watachukua mikoba kwa mda huu ambao klabu itakua ikitafuta kocha mwingine. Klabu hii inaenda kucheza mchezo wa kombe la FA na Leicester City jumapili hii katika uwanja wa Villa Park.
Aston Villa siku ya Jumanne alipigwa na Hull City 2-0 ambapo ni mechi ya 10 mfululizo katika ligi bila kushinda. Aston Villa kwasasa ipo nafasi ya 18 na ina pointi 22 tu katika Ligi Kuu Uingereza.



