Daily Archives: February 21, 2015

Klabu ya ES Setif yabeba Makombe yote ya Afrika mwaka 2014/2015….yachukua pia CAF SUPER CUP

Klabu ya Algeria ES SETIF ndo BINGWA wa CAF Super Cup. CAF Super Cup ni mchuano unaowakutanisha mshindi wa Bingwa Klabu Bingwa Afrika na Bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika. ES Setif ilikuwa ikicheza na Al Ahaly ya Misri katika uwanja wa Mustapha Tchaker. Kwa mwaka 2014/2015 ES Setif imeweza kuchukua Ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika na hili CAF Super Cup. ES Setif iliishinda klabu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kongo kwa goli la ugenini katika Fainali za Klabu Bingwa Afrika mwishoni mwa mwaka 2014.

B-Yr-AYIAAAKRRO

Read the rest of this entry

Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi daraja la kwanza kupigwa kesho Chamazi, Mwadui na African Sports kuumiza nyasi

Dar es Salaam:

Fainai za Kumsaka bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kupigwa kesho jumapili saa 10 Jioni kwa saa za hapa Tanzania. Mchezo huo ulitakiwa ufanyike uwanja wa Taifa, lakini Shirikisho la Soka Tanzania TFF limesema kuwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake mchezo utapigwa uwanja wa Chamazi.

Uwanja wa Chamazi Complex Dar es Salaam

Mchezo huo unatarajia kurushwa LIVE na kituo cha AZAM TV ili kuwafikia watu wengi mikoa mpambano huu mkali. Kinara ama Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza atajinyakulia kombe pamoja na medali, huku mshindi wa 2 atajipatia kikombe na medali pia.

Viingilio vya mchezo huo ni Tsh. 5,000 kwa jukwaa kuu na Tsh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.

Mwadui FC inashikilia msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza kundi la B ikiwa na pointi 46 katika michezo 22, huku African Sports inapointi 48 katika michezo 22 na yenyewe ikiwa ni kinara wa Ligi Daraja la Kwanza kundi A.

Design a site like this with WordPress.com
Get started