Monthly Archives: February 2015

Ivory Coast Bingwa Kombe la Mataifa Afrika 2015

Bata:

Ivory Coast ndo MABINGWA wapya wa Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2015. Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika 2015 yalifikia tamati katika uwanja wa Bata, Equatorial Guinea. Fainali hizi za tarehe 8/2/2015 zikiwakutanisha miamba wa Afrika Ghana na Ivory Coast wakimaliza dakika 120 za mchezo na kuingia katika mikwaju ya penati. Golikipa wa Ivory Coast Boubacar Barry ndo alionekana kama Mfalme wao baada ya kudaka penati ya kipa wa Ghana Brimah Razak kupiga penati ya mwisho iliyomshinda kipa wa Ivory Coast.

Ivory Coast ilishinda kwa penati 9 kwa 8 dhidi ya Ghana baada ya kumaliza dakika 120 za mchezo. Historia imejirudia ambapo Ivory Coast walishinda kwa penati 11-10 dhidi ya hawa Ghana. Hili ni kombe la pili la Ivory Coast kushinda.

Ivory Coast players

Ivory Coast ndo Mabigwa wa Kombe la Mataifa Afrika 2015

Boubacar Barry scores for Ivory Coast

Penati ya mwisho alopiga kipa Boubacar Barry na kuwapa Ubingwa Ivory Coast

Read the rest of this entry

Wenyeji Equatorial Guinea wanyimwa nafasi ya Tatu na Congo DR Kombe la Mataifa Afrika

Malabo:

Kutoka katika uwanja wa Malabo nchini Equatorial Guinea Mchezo uliokuwa unapigwa ni kuwania mshindi wa tatu katika Kombe la Mataifa Afrika. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CONGO DR) imeshika nafasi ya tatu kwa ushindi ulifika hatua ya kupigiana matuta. Congo DR imeshinda kwa mikwaju ya penati 4 kwa 2 dhidi ya Equatorial Guinea. Uwanja wa Malabo ulikuwa na mashabiki wachache sana kutoka na vurugu za mechi kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea. Mlinzi wa Congo DR Defender Cedric Mongongu ndo alipiga penati ya ushindi.

Embedded image permalink

kikosi cha Congo DR

Read the rest of this entry

Bingwa mara 4 wa Kombe la Mataifa Afrika atinga Fainali kwa kumpa kipigo kwake Equatorial Guinea kwa Vujo!

Kutoka Uwanja wa Malabo nchini Equatorial Guinea, mechi iliyokuwa inachezwa ni ya nusu fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2015. Mechi kati ya wenyeji Equatorial Guinea dhidi ya Ghana imemalizika kwa ushindi wa mgeni Ghana wa 3 kwa nunge. Ushindi uliosababisha Ghana kutinga fainali za Mataifa Afrika 2015 na atakutana na Ivory Coast hiyo Jumapili.

Ghana ni mabingwa wa Kombe hili mara nne kwa miaka ya  1963, 1965, 1978 na 1982, pia hii ni mara yao ya tano wanatinga Fainali hizi kwa miaka ya  1968, 1970, 1992, 2010 na sasa 2015. Ghana sasa kukipiga FAINALI na Ivory Coast siku ya Jumapili tarehe 8/2/2015 saa 4:00 usiku. Ivory Coast wao ni washindi wa kombe hili la Mataifa Afrika mara moja mwaka 1992 na wameshatinga fainali mara 3 mwaka wa 2006, 2012 na sasa 2015.

Photo: HATIMAYE MWAMUZI AMALIZA MPIRA UWANJA WA MALABO GHANA WATINGA FAINALI YA MATAIFA AFRIKA 2015
FT: Ghana 3 - 0 Equatorial Guinea

Read the rest of this entry

Dume lingine ya Uhispania, Barcelona kubadilisha jina la Uwanja wake Nou Camp

Uwanja wa klabu ya Barcelona unaweza kuja kubadilishwa jina lake la sasa Nou Camp hapo baadae. Mkataba na mdhamini wa Barcelona Qatar Airways unaenda kuisha mda wake mwaka 2016 ambao unathamani ya paundi milioni 25 kwa mwaka . Klabu ya Barcelona inayopatikana katika jimbo kubwa Catalunya nchini Uhispania hivi karibuni itafanya makubaliano na Qatar Airways ili kuongeza mkataba.

Uwanja wa Nou Camp

Mkurugenzi Mtendaji ama kwa kingereza CEO wa shirika la ndege la Qatar Airways amesema kuwa katika mkataba huo mpya jina la uwanja linaweza kubadilika kidogo kwa kuongezea maneno. Mkurugenzi wa shirika la ndege la Qatar, Bwana Akbar Al Baker ameendelea kusema kuwa katika mkataba huo jina la kampuni yaani QATAR linaweza kuongezwa kwenye jina la Uwanja Halisi NOU CAMP.

Read the rest of this entry

Kocha Hervé Renard Aipeleka Ivory Coast FAINALI za Kombe la Matiafa Afrika 2015 tena

Ivory Coast imetinga katika Fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2015 kwa kuitwanga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo goli 3 – 1 katika uwanja wa Bata. Ivory Coast sasa itakutana na Mshindi wa kati ya Equatorial Guinea na Ghana ambao watacheza tarehe 5/2/2015. Fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2015 zitapigwa siku ya Jumapili ya tarehe 8 mwezi huu

Ilikuwa ni vita ya Wafaransa wawili kocha J. Ikwanga-Ibenge na Herve Renard. Mechi ilikuwa ikitazamiwa kuwa ya ushindani mkubwa sana ukilinganisha uwezo wa wachezaji Bolasie, Mbokani, Makiadi na Bokila wote wa Kongo pamoja na mastaa wa Ivory Coast kama Gervihno, Bony, Yaya Toure na Kanon.

Mpira ulianza kwa lango la Kongo kushambuliwa kutoka kwa winga Gevihno na upenyo wa Yaya Toure. Akipokea pasi kutoka kwa Bony, Yaya Toure akafungua kalamu ya magoli dakika ya 20 kwa kukunjuka shuti lililokuwa linakadiliwa kuwa na spidi ya kilomita 125 kwa saa lililomshinda mlinda mlango wa Kongo Kidiaba, na mda mfupi dakika ya 22 Kongo wakapata penati iliyowekwa wavuni na Dieumerci Mbokani. Nae mchezaji wa zamani wa Arsenal Gervihno akapokea pasi kutoka kwa Wilfred Bony na akatupia la pili (2) dakika ya 40 likiwa pia ndo goli lake la 20 kwa Ivory Coast. Na kama haitoshi beki Serge Wilfried Kanon akashindilia msumari wa 3 ulioongezea kuwapeleka Ivory Coast kama Taifa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2015 huko Bata.

Embedded image permalink

Mchezaji wa Ivory Coast akifunga goli

Read the rest of this entry

Design a site like this with WordPress.com
Get started