Monthly Archives: February 2015

YANGA YAPANDA KILELENI MWA LIGI!

Yanga ama vijana wa Jangwani leo hii wamecheza mchezo wao wa 12 wa Ligi kuu Tanzania Bara. Yanga wamewafuata Tanga, Coastal Union leo hii na kuibuka na ushindi finyu wa goli moja kwa nunge katika uwanja wa Mkwakwani. Goli la Yanga limewekwa wavuni na Nahodha wao Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika dakika ya 12 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo. Ushindi huu umeifanya Yanga ikae kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 22 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 21 na inayaoshikilia nafasi ya tatu ni Mtibwa Sugar yenye pointi 18. Azam FC na Mtibwa Sugar wao washacheza michezo 11 kila moja.

vpl bar 1

Read the rest of this entry

Refa wa mechi ya Tunisia dhidi Equatorial Guinea ATIMULIWA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA 2015

Mkutano wa mkubwa uliofanyika makao makuu ya Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) huko Bata, Equatorial Guinea tarehe 2 Februari mwaka huu umechambua mchezo wa kombe la Mataifa Afrika kati ya Tunisia na Equatorial Guinea wa Tarehe 31 Januari 2015.

Kamati ya Marefa imegundua kuwa mchezo huo ulikuwa na mapungufu kwa upande wa refa (Mwamuzi wa kati) ambaye alionekana kushindwa kuchezesha mechi hiyo, hasa hasa kuwatuliza wachezaji waliokuwa na munkari.

Matokeo ya mechi namba 26 kati ya Tunisia na Equatorial Guinea

Kamati hiyo ya Waamuzi (marefa) imetoa maamuzi yafuatayo kwa mwamuzi Seechurn Rajindrapasard

  • Mwamuzi Seechurn Rajindrapasard ameachishwa kuchezesha mechi zilizobakia za Kombe la Mataifa Afrika 2015
  • Amesimamishwa kazi ya uamuzi kwa muda wa miezi 6.
  • Amefutwa kwenye Orodha ya Waamuzi wenye Sifa ya alama “A” ya CAF.

Read the rest of this entry

Hassan Isihaka na straika Ramadhan Singano Kukipiga Real Madrid?

Endapo watafanikiwa kucheza timu ya vijana ya klabu tajiri duniani, Real Madrid ya Uhispania, basi itakuwa ni habari njema kwa soka la Tanzania, ambayo wachezaji wake kadhaa wamekuwa wakifeli majaribio ya kucheza soka la kulipwa ughaibuni, hasa nchi za Ulaya katika miaka ya nyuma.

                                                     Wachezaji wa Simba

Kufuatia tetesi za kutakiwa kwenda kufanya majaribio Real Madrid, mashabiki wa soka wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam wamewaombea wachezaji wao kila la kheri katika majaribio yao ili waweze kusakata kabumbu Ulaya.

Haruna Hamisi, mmoja wa mashabiki na mwanachama wa Simba amesema beki wa kati wa klabu hiyo, Hassan Isihaka na straika Ramadhan Singano anayejulikana kama “Messi” kwa jina la uwanjani wana uwezo wa kucheza soka la kulipwa.

‘Vipaji tunavyo, ila vinakosa nafasi na kuharibiwa na mfumo wetu mbaya wa kutolea wachezaji wakiwa bado wadogo”, alisema Hamisi.

Read the rest of this entry

Kocha Harry Redknapp wa QPR AJIUZULU

                                                           Kocha Harry Redknapp

Kocha Harry Redknapp wa Klabu ya Queen Park Rangers ama “QPR” inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza ameachana nayo. Kocha huyo amesema kuwa ameachana na QPR kutokana na matatizo ya goti na anahitaji mda mwingi  ili afanyiwe upasuaji. Kocha huyo miaka 67 kawezi kutembea hata mita 100.

Harry Redknapp ameongea kwa simu na mwenyekiti wa QPR bwana Tony Fernandes. nakusema  ” Mimi sio mtu tena wa kuikoa QPR isishuke daraja na kwa masikitiko makubwa nahitaji nifanyiwe upasuaji wa haraka wa goti langu,” “kwa hili siwezi kutoa mchango wangu kwa timu wa asilimia 100, kunahitajika mtu wa kufanya hivyo” aliongeza.

Read the rest of this entry

Bei ya Kumnunua Cristiano Ronaldo: Wakala wake Jorge Mendes ATAJA!

                                                                       Cristiano Ronaldo

Wakala wa Mchezaji Maarufu wa Real Madrid Cristiano Ronaldo  aitwaye Jorge Mendes amesema kuwa kama kuna klabu inataka kumnunua basi itoe kiasi cha paundi milioni 300 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania 819,762,381,900.

Jorge Mendes amesema kuwa “Ronaldo ni mchezaji mzuri sana ambaye hajawahi tokea hivi karibuni katika hii dunia na huwezi kumshinddanisha na yoyote yule.” “Kama kuna kilabu kinamtaka basi kiandae paundi milioni 300,” aliongeza bwana Mendes.

Hata hivyo bwana Mendes amesema kuwa Ronaldo atabakia Real Madrid japo mapenzi yake kwa  mshabiki wake wa klabu yake ya zamani Manchester United ni makubwa sana.

Read the rest of this entry

Design a site like this with WordPress.com
Get started