Monthly Archives: March 2015

Tanzania yamuunga mkono Sepp Blatter Kinyang’anyiro cha Uraisi wa FIFA mwaka huu Mei.

Leo Rais wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) akiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wamezungumzia uchaguzi wa CAF na FIFA.

Rais Tenga ameishukuru familia ya TFF kwa kumuunga mkono katika kugombea tena nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF katika uchaguzi utakaofanyika Aprili 7 mwaka huu Cairo. Tenga ni mgombea pekee wa nafasi hiyo kwa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

0_0_0_0_427_320_csupload_63575827

Kutoka Kushoto Raisi wa TFF Jamali Malinzi, Raisi wa CAF Issa Hayatou na Leodegar Tenga

Pia Rais wa zamani wa TFF Leodgar Tenga amezungumzia msimamo wa bara la Afrika uliowekwa katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mwaka jana jijini Sao Paulo, Brazil kuwa wanachama wote wa CAF watamuunga mkono Rais wa sasa wa FIFA anayetetea nafasi yake katika uchaguzi utakaofanyika Mei mwaka huu jijini Zurich, Uswisi.

Vilevile Mkutano Mkuu wa CECAFA uliofanyika Desemba 2014 jijini Nairobi, Kenya ulipitisha azimio la kumuunga mkono Joseph Sepp Blatter katika uchaguzi wa FIFA. Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametoa tamko rasmi kuwa kwa niaba ya TFF atampigia kura Joseph Sepp Blatter.

Sepp Blatter kwa Ufupi.

Joseph “Sepp” Blatter ni raia wa nchi ya Uswisi mwenye miaka 79 sasa. Blatter amekuwa Raisi wa FIFA toka mwaka 1998. Mwaka huo wa 1998 alimpiku aliyekuwa raisi wa chama cha soka Barani Ulaya (UEFA) Lennart Johansson na kuchukua madaraka kutoka kwa bwana João Havelange. Kwa chaguzi za Uraisi wa FIFA, Blatter amechaguliwa mara nyingine 4 sasa (2002, 2007 na 2011) sasa 2015 itakua mara tano mfululizo.

Raisi wa FIFA Sepp Blatter

Blatter amekuwa akiandamwa na kashifa nyingi za rushwa, kufuja mali za FIFA na ikiwemo kashfa kubwa ya kubariki kombe la dunia huko Qatar mwaka 2022 kinyume na utaratibu.

Wapinzani wa Sepp Blatter mwaka huu 2015 ni Luis FigoJerome Champagne, Prince Ali bin Al-Hussein na Michael van Praag.

  • Issa Hayatou raia wa Kamerunimwenye umri wa miaka 68 amekuwa Raisi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) toka mwaka 1988.

BODI YA LIGI KUU YATOA ADHABU ZIFUATAZO BAADA YA KUKAA KWENYE KIKAO JUMANNE NA KUPITIA TAARIFA MBALI MBALI ZA MICHEZO

Kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu kilichoketi Jumanne ya tarehe 24 mwezi huu wa 3, 2015 kimepitia taarifa
mbalimbali za michezo na kutoa adhabu kemi kem zifuatazo;

image

Katika mechi namba 107 iliyowakutanisha wenyeji
Ndanda FC dhidi ya Coastal Unioni, klabu ya
Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano)
kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu ya
Vodacom  kutokana na washabiki wake kumrushia
chupa za maji mwamuzi msaidizi Anold Bugado.
Mechi namba 108 iliyochezwa Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga, (Stand United dhidi
Simba SC), wenyeji timu ya Stand United imepigwa
faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa
Kanuni ya 14(8) kutokana na timu yake kuchelewa
kufika uwanjani kwa dakika ishirini.

Read the rest of this entry

Ratiba ya Leo | Today Mega Fixture 14, March 2015

Ratiba ya leo | Mega Fixture 14, march 2015
** Premier League
3:45 PM Crystal Palace vs Queens Park Ra…
6:00 PM Arsenal vs West Ham United
6:00 PM Leicester City vs Hull City
6:00 PM Sunderland vs Aston Villa
6:00 PM West Bromwich … vs Stoke City
8:30 PM Burnley vs Manchester City
** France – Ligue 1
7:00 PM Metz vs Saint-Étienne
10:00 PM Lens vs Toulouse
10:00 PM Lorient vs Caen
10:00 PM Montpellier vs Reims
10:00 PM Nantes vs Evian TG
** Germany – Bundesliga
5:30 PM Augsburg vs Mainz 05
5:30 PM Hoffenheim vs Hamburger SV
5:30 PM Hertha BSC vs Schalke 04
5:30 PM Werder Bremen vs Bayern München
5:30 PM Eintracht Fran… vs Paderborn
8:30 PM Borussia Dortmund vs Köln
** Italy – Serie A
8:00 PM Palermo vs Juventus
10:45 PM Cagliari vs Empoli
** Spain – Primera División
6:00 PM Espanyol vs Atlético Madrid
8:00 PM Eibar vs Barcelona
10:00 PM Rayo Vallecano vs Granada
12:00 AM Celta de Vigo vs Athletic Club

Soma kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya michezo hapa Tanzania

.

DSC00415

Read the rest of this entry

RATIBA YA EUROPA LEAGUE LEO | 12, March

Europe – UEFA Europa League
8:00 PM (20:00) Zenit vs Torino
9:00 PM (21:00) Dnipro Dniprop…vs Ajax
9:00 PM (21:00) Wolfsburg vs Internazionale
9:00 PM (21:00) Club Brugge vs Beşiktaş
11:05 PM (23:05) Everton vs Dynamo Kyiv
11:05 PM (23:05) Villarreal vs Sevilla
11:05 PM (23:05) Napoli vs Dinamo Moskva
11:05 PM (23:05) Fiorentina vs Roma

Design a site like this with WordPress.com
Get started