Monthly Archives: April 2015

Tanzania na Rwanda kuwa wenyeji wa michuano ya CECAFA 2015.

Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa michuano ya Kagame ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi julai katika jijini la Dar es Salaam mwaka huu 2015. Na michuano ya kombe Challenge inatarajia kupigwa jijini Kigali mwezi Novemba baada ya Rwanda kuchagiliwa na Cecafa mwaka huu.

Uamuzi huo umefikiwa jijini Nairobi kwenye mkutano wa kamati ya Cecafa siku ya Jumanne. Mkutano huo ulihudhuriwa na raisi wa Cecafa Leodegar Tenga, katibu mkuu  Nicholas Musonye, Raisi wa Shirikisho la soka Uganda Moses Magogo, Raisi wa Shirikisho la soka Kenya Sam Nyamweya na  Raisi wa Shirikisho la soka Tanzania Jamal Malinzi.

Michuano ya kombe la Challenge haikufanyika mwaka uliopita kutokana na Wenyeji Ethiopia kujitoa kwenye michuano dakika za mwisho. Kwa upande wa Kagame Al Merreikh ya Sudani ilitawazwa Bingwa baada ya kumpiga mwenyeji APR 1-0 jiji Kigali. Harambee Stars walikuwa mabingwa mwaka 2013 kwa kuifunga Falcons ya Sudani 2-0 katika uwanja wa Nyayo.

Wakati huo huo Cecafa chini ya miaka 17 itaanza kutimua vumbi mwaka huu kuanzia August na Octoba mwenyeji akiwa ni Uganda.

Makundi ya Kufuzu Kombe la Mataifa Afrika 2017 yapangwa..Kenya, Tanzania, Rwanda na Burundi wapo makundi mazito.

Upangaji wa makundi ya Kufuzu kombe la Mataifa Afrika 2017 umekamilika leo hii tarehe 8, Aprili huko jijini Cairo, Misri. Jumla ya nchi 52 kutoka katika kundi A mpaka M za Afrika zinatarajia kushiriki michuano hii ambayo itaanza kutimua vumbi mwaka huu 2015 terehe za 12,13 na 14 mwezi wa 6.

Kwa mara nyingine tena kutoka Afrika Magharibi nchi ya Gabon ndio imetangazwa na Raisi wa CAF bwana  Issa Hayatou kuwa nchi mwenyeji wa Michuano hii 2017 kutoka katika kura iiyopigwa na kamati kuu ya utendaji ya CAF. Gabon ilikuwa nchi mwenyeji wa michuano hii kwa mwaka 2012 pamoja na  Equatirial Guinea. Gabon imezipiku Ghana na Algeria kuandaa michuano hii ya Kombe la Mataifa Afrika ya 31.

Gabon named hosts of AFCON 2017

Raisi wa CAF Issa Hayatou

Read the rest of this entry

Design a site like this with WordPress.com
Get started