Daily Archives: April 18, 2015
Tanzania na Rwanda kuwa wenyeji wa michuano ya CECAFA 2015.
Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa michuano ya Kagame ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi julai katika jijini la Dar es Salaam mwaka huu 2015. Na michuano ya kombe Challenge inatarajia kupigwa jijini Kigali mwezi Novemba baada ya Rwanda kuchagiliwa na Cecafa mwaka huu.
Uamuzi huo umefikiwa jijini Nairobi kwenye mkutano wa kamati ya Cecafa siku ya Jumanne. Mkutano huo ulihudhuriwa na raisi wa Cecafa Leodegar Tenga, katibu mkuu Nicholas Musonye, Raisi wa Shirikisho la soka Uganda Moses Magogo, Raisi wa Shirikisho la soka Kenya Sam Nyamweya na Raisi wa Shirikisho la soka Tanzania Jamal Malinzi.
Michuano ya kombe la Challenge haikufanyika mwaka uliopita kutokana na Wenyeji Ethiopia kujitoa kwenye michuano dakika za mwisho. Kwa upande wa Kagame Al Merreikh ya Sudani ilitawazwa Bingwa baada ya kumpiga mwenyeji APR 1-0 jiji Kigali. Harambee Stars walikuwa mabingwa mwaka 2013 kwa kuifunga Falcons ya Sudani 2-0 katika uwanja wa Nyayo.
Wakati huo huo Cecafa chini ya miaka 17 itaanza kutimua vumbi mwaka huu kuanzia August na Octoba mwenyeji akiwa ni Uganda.

