Daily Archives: December 10, 2015
TP Mazembe apata atakae chuana nae huko japani
Mabingwa wa Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo watakutana na timu ya Sanfrecce Hiroshima kutoka Japan Kombe la Dunia la Klabu Jumapili. Hii ni baada ya matokeo haya
SANFRECCE HIROSHIMA 2-0 AUCKLAND CITY (magoli na Y Minagawa 9′ na T. Shiotani 70′)
Mshindi wa mechi kati ya Mazembe na Hiroshima atakutana na mabingwa wa Amerika Kusini River Plate ya Argentina nusufainali Desemba 16.
Arsenal sasa hatua ya Mtoano, 16 bora
Arsenal katika usiku wa Klabu Bingwa Ulaya ilikua inahitajika kushinda goli 2-0 au 3-2 ili kuendelea na hatua ya mtoano. Goli 3 za Olivier Giroud zilihakikishia Arsenal wanaoshika nafasi ya 2 Ligi Kuu England kufika hatua ya mtoano yaani (Hatua ya 16 bora). Hata hivo Arsenal yaweza kukabiliwa na kibarua kizito wakati wa upangaji wa makundi hiyo Jumatatu, inaweza pangwa na Real Madrid, Barcelona, Wolfsburg au Zenit St Petersburg. Timu za England zikizosonga mbele ni Arsenal, Chelsea na Manchester City, Manchester United ilitolewa katika michuano hii.


