Monthly Archives: November 2016
AFRIKA KUSINI, GHANA MATUMAINI YATOWEKA, HUKU WATAKAO CHUANA FAINALI WAKIJULIKANA..KOMBE LA MATAIFA AFRIKA KWA WANAWAKE
Hatimaye fainali ya kombe la mataifa Afrika kwa wanawake yafikia patamu baada ya nchi mbili kutinga fainali. Fainali hii itashuhudiwa siku ya jumamosi hii huko Cameroon.
Mechi za nusu fainali zimechezwa leo hii huku timu nne zikishuka dimbani kupambana kutinga fainali. Wenyeji Cameroon wamechuana na Ghana huku Nigeria wakimenyana vikali na Afrika Kusini.
NUSU FAINALI YATAFUTWA KWA NGUVU HUKO CAMEROON…
Jana michezo ya kundi A ilipigwa kukamilisha hatua ya makundi huko nchini Kameruni. Nusu fainali yatafutwa kwa nguvu huku vipigo vikali vikionekana.
Mechi ya kwanza ilishuhudiwa wenyeji Cameroon kushinda dhidi ya Zimbabwe 2-0. Ushindi huo umeifanya Cameroon kushinda mechi zote za makundi na kuibuka na alama zote 9. Zimbabwe wao wametolewa kwenye mashindano Kwa kuondoka na alama moja tu aliyoipata kwa kutoka 0-0 na Afrika Kusini.
KENYA WAUMIA TENA, HUKU NIGERIA NA GHANA WAKITUNISHIANA MISURI…
Kundi B Jana limeingia duru ya 2 ambapo Nigeria wamekutana na Ghana nao Kenya wakiwa dhidi ya Mali.
Kutoka uwanja wa Manisipaa ya Limbe nchini Cameroon, Nigeria imetoka 1-1 dhidi ya Ghana, ambapo Nigeria imepata bao kupitia kwa Asisat Oshoala kwa shuti zuri la adhabu ndogo. Elizabeth Addo akiifungia Ghana dak ya 44. Asisat Lamina Oshoala miaka 22 anaongoza kwa magoli 5 katika hii michuano.Asisat sasa anaichezea timu ya wanawake ya Arsenal akiwa na jezi namba 24.
Mchezo mwingine umehusika kwa Kenya kufungwa 3-1 na Mali. Kenya kwa matokeo haya imetolewa katika mashindano ikisubiri kukamilisha ratiba tu.
Msimamo kundi B
- Nigeria alama 4
- Ghana alama 4
- Mali alama 3
- Kenya alama 0
CAMEROON MIGUU YOTE NDANI KOMBE LA MATAIFA AFRIKA KWA WANAWAKE..ZIMBABWE, MISRI NA AFRIKA KUSINI?
Jana mechi za pili zilipigwa huko Yaounde Kameruni uwanja wa Ahmadou Ahidjo kwa kundi A. Cameroon imeshinda zote mbili na kutimua vumbi kuwaacha wapinzani wake hadi kutinga nusu fainali za mashindano haya.
Wenyeji Cameroon wameweza tumia uwenyeji wao vizuri baada ya kumfunga Afrika Kusini 1-0 dak za lala salama (83′) kupitia kwa Genevieve Ngo. Kipigo hicho kwa Afrika kusini kimemweka kocha Desiree Ellis katika haki ngumu ya kufika nusu fainali. Afrika ya kusini ilitoa droo tasa na kuondoka alama moja dhidi ya Zimbabwe katika mchezo namba moja. Afika kusini sasa kukabiliana na Misri siku ya ijumaa hii.
Mchezo mwingine wa kundi B ulikua kati ya Zimbabwe dhidi ya Misri. Mchezo huu umeisha kwa Misri kuibuka na ushindi wa 1-0 goli likiwekwa kwa nyavu na Salma Tarik dak ya 83. Goli la Salma limefanya Misri iibuke na alama 3 muhimu zilizowapa matumaini ya kusonga mbele zaidi. Zimbabwe kukabiliana vikali na Cameroon siku ya ijumaa pia.
Msimamo kundi A
- Cameroon alama 6
- Misri alama 3
- Zimbabwe alama 1
- Afrika Kusini alama 1
Kwa matokeo ya jana Kameruni ametinga nusu fainali za mataifa Afrika kwa wanawake 2016 huku Zimbabwe, Misri na Afrika Kusini wakisubiri ijumaa ilikufanya jitihada.
Mechi za leo 23/11/2016 ni za Kundi B
- Nigeria vs Ghana
- Kenya vs Mali
Nigeria na Ghana wote wana alama 3 kila moja wakati Kenya na Mali wote wana alama 0.
KOMBE LA MATAIFA AFRIKA KWA WANAWAKE..KENYA NA MALI WAONJA MASHINDANO KATIKA STAILI YA PEKEE


Mashindano ya mataifa Afrika Kwa wanawake yaingia duru ya pili hiyo Jana kwa wanawake kutoka Nigeria, Mali, Ghana na Kenya ya Afrika ya mashariki kuwakilisha mataifa yao katika kundi B. Mechi zimepigwa katika dimba la Manisipaa ya Limbe, jijini Limbe.
Mechi ya kwanza iliwakutanisha Nigeria Bingwa mtetezi dhidi ya Mali. Nigeria imemtwanga Mali 5-0. Nigeria ilitawala mchezo ambapo mfungaji ambae kwa sasa anaongoza Kwa magoli Asisat OShoala akitupia 4 peke yake dak ya 40, 63, 68 na 77. Magoli mengine yamefungwa na Ordega Francisca dak ya 21 na Uchachi Sunday dak ya 47.
Mechi nyingine ilikua kati ya Ghana dhidi ya Kenya. Ghana iliweza kumshinda Kenya aliyecheza mchezo mzuri goli 3-1. Kalamu ya magoli ilifunguliwa na Kenya dak 22 na Essie Akida. Ghana kipindi cha pili waliweza kuusoma mchezo na kufunga goli dak ya 50 na Samira Suleiman, dak ya 72 Portia Boakye akafunga kwa mkwaju wa penati na Elizabeth Addo akafunga la mwisho dak ya 89.
Kwa michezo ya jana ya kundi B Nigeria inaongoza kwa alama 3, ikifuatiwa na Ghana alama 3, huku Kenya na Mali wakifuata kwa mfululizo wakiwa wana alama 0.
MATOKEO MECHI ZA KWANZA KUNDI B
- Nigeria 6-0 Mali
- Ghana 3-1 Kenya

