Daily Archives: November 19, 2016
KOMBE LA MATAIFA AFRIKA KWA WANAWAKE 2016 LAANZA RASMI
Kombe la Mataifa Afrika kwa wanawake limeanza rasmi hii leo huko Cameroon. Kombe hili limeshuhudiwa katika jiji la Younde huku jiji la Kimbe kikisubiria mechi zijazo. Mechi 2 zimeanza kukipiga na matokeo ni haya hapa:
- Cameroon 2-0 Misri
- Afrika Kusini 0-0 Zimbabwe
Wenyeji Cameroon wamepata ushindi wao wa kwanza katika hatua hii ya makundi kupitia kwa Gabrielle Aboudi na Christine Manie kupitia mkwaju wa penati. Mechi nyingine ilikua ni Afrika kusini dhidi ya Zimbabwe ambapo wametoka kwa tasa isiyo na goli.
Timu zinazowakilisha katika haya mashindano ni 8 makundi 2 na yameanza kutimua vumbi hii leo 19, Novemba mpaka 3, Desemba 2016. Mabingwa watetezi ni Nigeria wakiongoza pia kwa kuwa na makombe mengi 9 kuliko nchi yoyote ile.
Kundi A
- Cameroon
- Misri
- Afrika Kusini
- Zimbabwe
Kundi B
- Ghana
- Kenya
- Mali
- Nigeria.

