Daily Archives: November 20, 2016

KOMBE LA MATAIFA AFRIKA KWA WANAWAKE..KENYA NA MALI WAONJA MASHINDANO KATIKA STAILI YA PEKEE

Uploading…

​Mashindano ya mataifa Afrika Kwa wanawake yaingia duru ya pili hiyo Jana kwa wanawake kutoka Nigeria, Mali, Ghana na Kenya ya Afrika ya mashariki kuwakilisha mataifa yao katika kundi B. Mechi zimepigwa katika dimba la Manisipaa ya Limbe, jijini Limbe.

Mechi ya kwanza iliwakutanisha Nigeria Bingwa mtetezi dhidi ya Mali. Nigeria imemtwanga Mali 5-0. Nigeria ilitawala mchezo ambapo mfungaji ambae kwa sasa anaongoza Kwa magoli Asisat OShoala akitupia 4 peke yake dak ya 40, 63, 68 na 77. Magoli mengine yamefungwa na Ordega Francisca dak ya 21 na Uchachi Sunday dak ya 47.

Mechi nyingine ilikua kati ya Ghana dhidi ya Kenya. Ghana iliweza kumshinda Kenya aliyecheza mchezo mzuri goli 3-1. Kalamu ya magoli ilifunguliwa na Kenya dak 22 na Essie Akida. Ghana kipindi cha pili waliweza kuusoma mchezo na kufunga goli dak ya 50 na Samira Suleiman, dak ya 72 Portia Boakye akafunga kwa mkwaju wa penati na Elizabeth Addo akafunga la mwisho dak ya 89.

Kwa michezo ya jana ya kundi B Nigeria inaongoza kwa alama 3, ikifuatiwa na Ghana alama 3, huku Kenya na Mali wakifuata kwa mfululizo wakiwa wana alama 0.

MATOKEO MECHI ZA KWANZA KUNDI B

  • Nigeria 6-0 Mali
  • Ghana 3-1 Kenya
Design a site like this with WordPress.com
Get started