Daily Archives: November 22, 2016

CAMEROON MIGUU YOTE NDANI KOMBE LA MATAIFA AFRIKA KWA WANAWAKE..ZIMBABWE, MISRI NA AFRIKA KUSINI?

​Jana mechi za pili zilipigwa huko Yaounde Kameruni uwanja wa Ahmadou Ahidjo kwa kundi A. Cameroon imeshinda zote mbili na kutimua vumbi kuwaacha wapinzani wake hadi kutinga nusu fainali za mashindano haya.

Wenyeji Cameroon wameweza tumia uwenyeji wao vizuri baada ya kumfunga Afrika Kusini 1-0 dak za lala salama (83′) kupitia kwa Genevieve Ngo. Kipigo hicho kwa Afrika kusini kimemweka kocha Desiree Ellis katika haki ngumu ya kufika nusu fainali. Afrika ya kusini ilitoa droo tasa na kuondoka alama moja dhidi ya Zimbabwe katika mchezo namba moja. Afika kusini sasa kukabiliana na Misri siku ya ijumaa hii.

​Mchezo mwingine wa kundi B ulikua kati ya Zimbabwe dhidi ya Misri. Mchezo huu umeisha kwa Misri kuibuka na ushindi wa 1-0 goli likiwekwa kwa nyavu na Salma Tarik dak ya 83. Goli la Salma limefanya Misri iibuke na alama 3 muhimu zilizowapa matumaini ya kusonga mbele zaidi. Zimbabwe kukabiliana vikali na Cameroon siku ya ijumaa pia.

Msimamo kundi A

  1. Cameroon alama       6
  2. Misri alama                  3
  3. Zimbabwe alama       1
  4. Afrika Kusini alama 1

 Kwa matokeo ya jana Kameruni ametinga nusu fainali za mataifa Afrika kwa wanawake 2016 huku Zimbabwe, Misri na Afrika Kusini wakisubiri ijumaa ilikufanya jitihada.

Mechi za leo 23/11/2016 ni za Kundi B

  • Nigeria vs Ghana
  • Kenya vs Mali 

Nigeria na Ghana wote wana alama 3 kila moja wakati Kenya na Mali wote wana alama 0.

Design a site like this with WordPress.com
Get started