Daily Archives: November 23, 2016

KENYA WAUMIA TENA, HUKU NIGERIA NA GHANA WAKITUNISHIANA MISURI…

Kundi B Jana limeingia duru ya 2 ambapo Nigeria wamekutana na Ghana nao Kenya wakiwa dhidi ya Mali.

​Kutoka uwanja wa Manisipaa ya Limbe nchini Cameroon, Nigeria imetoka 1-1 dhidi ya Ghana, ambapo Nigeria imepata bao kupitia kwa Asisat Oshoala kwa  shuti zuri la adhabu ndogo. Elizabeth Addo akiifungia Ghana dak ya 44. Asisat Lamina Oshoala miaka 22 anaongoza kwa magoli 5 katika hii michuano.Asisat sasa anaichezea timu ya wanawake ya Arsenal akiwa na jezi namba 24.

​Mchezo mwingine umehusika kwa Kenya kufungwa 3-1 na Mali. Kenya kwa matokeo haya imetolewa katika mashindano ikisubiri kukamilisha ratiba tu.

Msimamo kundi B

  1. Nigeria alama 4
  2. Ghana alama 4
  3. Mali alama 3
  4. Kenya alama 0
Design a site like this with WordPress.com
Get started