Monthly Archives: November 2016

KOMBE LA MATAIFA AFRIKA KWA WANAWAKE 2016 LAANZA RASMI

​​Kombe la Mataifa Afrika kwa wanawake limeanza rasmi hii leo huko Cameroon. Kombe hili limeshuhudiwa katika jiji la Younde huku jiji la Kimbe kikisubiria mechi zijazo. Mechi 2 zimeanza kukipiga na matokeo ni haya hapa:

  • Cameroon 2-0 Misri
  • Afrika Kusini 0-0 Zimbabwe 

Wenyeji Cameroon wamepata ushindi wao wa kwanza katika hatua hii ya makundi kupitia kwa Gabrielle Aboudi na Christine Manie kupitia mkwaju wa penati. Mechi nyingine ilikua ni Afrika kusini dhidi ya Zimbabwe ambapo wametoka kwa tasa isiyo na goli.

Timu zinazowakilisha katika haya mashindano ni 8 makundi 2 na yameanza kutimua vumbi hii leo 19, Novemba mpaka 3, Desemba 2016. Mabingwa watetezi ni Nigeria wakiongoza pia kwa kuwa na makombe mengi 9 kuliko nchi yoyote ile.

Kundi A

  1. Cameroon
  2. Misri
  3. Afrika Kusini
  4. Zimbabwe

Kundi B

  1. Ghana
  2. Kenya
  3. Mali
  4. Nigeria.

JICHO LETU LEO

Wapo wachezaji wengi sana tumekua tukiwafatilia wakifanya maajabu tokea hapo wakiwa wadogo mpaka wanapokua wakubwa. Nyota hao wameweza kushangaza dunia sana mno, kwa wale waliowaona nyota hao wakiwa bado wadogo…ni dhahiri shahiri kipindi hicho watu hao walisema “huyu Dogo atakua nyota wa dunia katika Soka”.

Na leo katika JICHO LETU kwa ufupi kabisa tunae Karamoko Kader Dembele. Karamoko Dembele ali maarufu kama “Kaddy” ni mchezaji ambae nae anapitia katika njia waliopita nyota wakubwa wa dunia hii ya leo. Karamoko Dembele ni kinda wa kipekee miaka 13 anaetumia guu la kushoto kama nyota wa zamani waliokuna walimwengu Lionel Messi, Maradona, Nilton Santos, Ferenc Puskas, Ryan Giggs na wengine wengi.

Read the rest of this entry

Design a site like this with WordPress.com
Get started