Monthly Archives: December 2016
Nigeria mabingwa tena, hawakamitiki Afrika…..
Kombe la mataifa Afrika 2016 leo limefikia tamati kwa fainali ya Nigeria dhidi ya wenyeji Cameroon. Mchezo umeshuhudiwa na raisi wa Cameroon Paul Biya na mashabiki takribani 40,000 huku ulinzi ukiwa mkali.
Nigeria imechukua Ubingwa kupitia kwa goli la mfungaji bora wa kombe hili la mwaka 2014 Desire Oparanozie akipokea pasi kutoka kwa mchezaji bora wa kombe hili la 2014 Asisat Oshoala dak ya 84.
