Monthly Archives: January 2017
GHANA HAOO WAWAFUATA SENEGAL ROBO FAINALI HUKU WAPIGANAJI WA UGANDA WATOLEWA NA MISRI DAKIKA ZA MWISHO!
Mechi za kundi D zilipigwa hiyo Jana kukamilisha hatua ya makundi kwa awamu ya 2 ikiwa imesalia awamu moja tu.
Mchezo wa kwanza ulihusisha Ghana dhidi ya Mali. Ghana iliingia uwanjani ikiwa na alama 3 baada ya mchezo wake wa kwanza kumfunga Uganda, huku Mali ikiwa na alama moja baada ya kutoka bila kufungana na Misri. Ghana ilianza vizuri kwa kushambulia huku wanadinga wake kama J. Ayew, A. Ayew na Gyan wakifika langoni kwa Mali kila mara. Dak ya 21 Straika Asamoah Gyan akafunga bao pasi ya goli ikitoka kwa Jordan Ayew. Sasa Ghana ya Mwisraeli Avram Grant kupepetana na Misri huku tayari ikiwa ishajihakikishia nafasi hatua ya Robo fainali.
WAPIGANAJI WA JANGWANI HALI TETE WAKATI SIMBA WA TERANGA WATINGA ROBO FAINALI
Kundi B lilitinga dimbani Jana katika uwanja wa Franceville, Gabon huku matokeo yakishangaza wengi.
Mchezo wa kwanza ulikua ni Algeria dhidi ya Tunisia. Mahasimu hawa wa Afrika ya kaskazini walikutana huku Tunisia ikiibuka na ushindi wa kwanza wa mashindano haya ya 2017.
Dakika ya 50 Aissa Mandi wa Algeria akajifunga huku faida ikienda kwa Tunisia. Baadae dak ya 65 wakapata pigo tena wapiganaji wa Jangwani ama Algeria baada ya Gloulam kumwangusha Khazori kwenye boksi na mwamuzi kutoka ushelisheli kuamua kupigwa penati na kujazwa golini na Sliti Naim.

Dak ya 90 kabla ya kuongezwa dak za nyongeza Algeria wakiongozwa na mwanadinga Mahrez wakafanya shambulizi la kushitukiza na hatimaye dak ya 90+1 wakapata bao kupitia kwa mpiganaji wa jangwani Sofiane Hanni
WAKONGO WATUMWA KUFANYA KAZI, ADEBAYOR NA ZAHA NGOMA DROO!
Kundi C kombe la mataifa Afrika lilishuka dimbani kuziwakilisha nchi zao hiyo Jana. Ivory Coast dhidi ya Togo na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo dhidi ya Morocco.
Mchezo wa kwanza uliowakutanisha wanadinga wakali na maarufu kama Sheyi Emmanuel Adebayor, Wilfred Bony, Solomoni Kalou, Zaha n.k ulikua kati ya Ivory Coast na Togo. Mchezo huu uliisha kwa 0-0.
SIMBA WA TERANGA WAJA KWA KASI AFCON 2017, HUKU MAHREZ AKIOKOA ALGERIA!
Kombe la mataifa Afrika limeingia duru ya pili hiyo Jana huko Francville, Gabon. Kundi B ambalo limeundwa na bingwa wa 2004 Tunisia, Algeria, Zimbabwe na Senegal.
Mechi ya mapema zaidi ilikua kati ya Zimbabwe dhidi ya Algeria. Mchezaji bora wa Afrika 2016 na kiungo wa Leicester City Riyad Mahrez alianza kuona lango la wapinzani wake dak ya 12 na kuwaacha Zimbabwe wakiduwaa. Zimbabwe iliwachukua dak 5 kurudisha goli kupitia kwa Mahachi dak ya 17 ya mchezo. Na kama haitoshi dak ya 29 Mushakwi akapiga goli safi la kichwa. Mpaka Mapumziko Zimbabwe ilikua ikiongoza 2-1. Kipindi cha pili Algeria walifanya mashambulizi ya nguvu huku Zimbabwe wakitumia mda wote kwa kulinda lango. Hatimaye Mahrez akasawazisha dak ya 82 na kuondoka na alama moja.
KOMBE LA MATAIFA AFRIKA LAANZA NA DROO! UFUNGUZI WAFANA!
Pazia la Kombe la mataifa Afrika 2017 limefunguliwa rasmi huko nchini Gabon kwa wenyeji kucheza mchezo wao Wa kwanza na Guinea-Bissau, huku mahasimu wao Cameroon wakichuana vikali na Burkana Faso (Burkinebe).
Mashindano haya yanayodhaminiwa na kampuni la Total yalianza kwa shamara shamra za wasanii mbali mbali kutumbuiza. Moja ya msanii kutoka Tanzania ni Diamond Platnum ambaye alitumbuiza kwa mara ya kwanza na kuweka historia kwa mwanamziki kutoka Afrika Mashariki kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano haya.

Diamond Platnum akitumbuiza mashabiki AFCON 2017



