Daily Archives: July 8, 2017
MCHEZAJI AJAX AANGUKA UWANJANI NA KUKIMBIZWA HOSPITALI
Kiungo mdachi wa Ajax Abdelhak Nouri (20) mwenye asili ya Morocco ameanguka mapema hii leo na kukimbizwa hospitali kwa helikopta baada ya kutibiwa uwanjani kwa dak 10 bila mafanikio. Nouri alikua akicheza mchezo wa kirafiki akiwa na timu yake ya Ajax dhidi ya Werder Bremen.
Tukio hilo limesababisha mtanange kuhairishwa ambapo imemkuta kiungo huyo kipindi cha pili huko Austria.
Ikumbukwe Nouri alikua kwenye kikosi kilichosafiri mpaka Stockholm kwa mchezo wa fainali ya Uropa dhidi ya Manchester United.
Wachezaji wengi wametuma salamu za apone haraka akiwemo nahodha wa zamani wa Netherland Ruud Gullit.
Taarifa kutoka akaunti ya twitter ya Ajaxdaily imeripoti kuwa Nouri alipatwa na mshitukowa moyo uliopelekea mapigo kutoenda ipasavyo. Kwasasa anaendelea vizuri.
Mtandao wa Soccercaster unamtakia apone haraka.

